RC Chalamila awasha moto wanaohujumu kahawa

MKUU wa Mkoa wa Kagera Alberth Chalamila  amesema atakula sahani moja na watumishi wanaoshirikiana na wafanyabiashara wasio waaminifu kwa kupokea rushwa ili kuwarhusu kusafirisha Kahawa nje ya nchi bila kufuata utaratibu.

Akizungumza wakati wa ziara yake wilayani Kyerwa eneo la Murongo  ambapo ni lango kuu la kuingilia nchi za Uganda, Congo na Sudani Kusini, Chalamila ameonya watumishi wanaosaliti serikali kwa kupokea rushwa ili kuruhusu magendo akisema dawa yao iko jikoni.

Alisema kwa miaka mingi  kuna baadhi ya wafanyabiashara wasiotaka kubadilika.  Kazi yao kubwa ni kupokea rushwa, amesema akitaja watumishi hao kuwa ni pamoja na wale wa Halmashauri, watumishi wa mipakani, baadhi ya askari polisi na Mgambo.

“Nina ukurasa na majina ya wafanyabiashara wanaofanya Magendo.  Kwa bahati mbaya hata vyombo vya dola wengine labda haviwaoni, Nina majina ya watumishi ambao wanahusika na wanaotumika kama kinga kuwalinda wafanyabiashara. Kuna baadhi ukitangaza wajisalimishe wanapiga simu juu. Nawatumia salamu leo hii, tutakula sahani moja hamuwezi kuendelea kuwa wasaliti wa nchi yetu,” amesema Chalamila.

RC Chalamila amesema yuko tayari kufuta makosa yaliyojitokeza huko Nyuma na kufungua ukurasa mpya kwa wafanyabiasha walio tayari kubadilika nakuacha njia za Magendo na kufanya Biashara halali.

Aidha alisema serikali inatatua changamoto ya Barabara  kwa  kujenga barabara ya Murongo  Hadi Omugakorongo kwa  kiwango cha lami, ujenzi wa kituo Cha pamoja cha forodha katika mpaka wa Murongo, upanuzi na ujenzi wa Daraja jipya la mto Kagera katika mpaka wa Murongo pamoja na  ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami kutoka Omurushaka kuja Murongo kilometa 50.

Mbunge wa Jimbo la Kyerwa Inocent Bilakwate alimwambia mkuu wa mkoa kuwa endapo serikali itaweza kuwabaini watumishi  wasaliti walioajiliwa na serikali kiwango kikubwa cha kahawa  hakitapelekwa nchi jirani kwa Magendo hivyo takwimu za uzalishaji zitapanda.

 

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button