RC Mogela atoa maelekezo hoja za CAG

MKUU wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amewaagiza wakuu wa idara na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru kusimamia ujibuji wa hoja za Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa ufasaha na kuambatanisha nyaraka za uthibitisho, ili kufuta hoja hizo.

Mongella ametoa Maagizo hayo kwenye kikao maalum cha Baraza la Madiwani cha kujadili Hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali za halmashuri ya Wilaya ya Meru wa mwaka wa fedha 2021/2022.

Pia amesesitiza ukusanyaji wa mapato upewe kipaumbele, ambapo ameelekeza fedha za makusanyo kuwekwa benki kwa wakati pamoja na halmashauri kuongeza umakini katika kuchagua na kuwaajiri vibarua wa kukusanya mapato, ili kuepuka ukusanyaji hafifu wa mapato hususan kwenye soko la Tengeru.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button