RC Sendiga awahimiza Wahadzabe uchaguzi mitaa

MKUU wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga ameihimiza jamii ya Wahadzabe inayoishi kijiji cha Mongo-Wa-Mono wilayani Mbulu kujiandikisha katika daftari za makazi ili kuchangua viongozi wanaowataka katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

RC Sendiga amefika kijijini hapo katika akiwa na zawadi ya kitoweo cha nyama ya nyumbu ili kuishawishi jamii hiyo kuwa na utulivu wa muda na kwenda kujiandikisha katika daftari la makazi kabla ya zoezi hilo kufikia ukomo leo.

Advertisement

Akizungumza kijijini hapo, RC Sendiga amewasihi kushiriki kuwachagua viongozi wa jamii yao wenye uwezo wa kuwaongoza kuharakisha juhudi za maendeleo katika eneo lao.

Wakizungumza kwa niaba ya wenzao, Salum Joseph Duduqwe na Zuberi Mathayo wamemshukuru kiongozi huyo kwa kuwatembelea ambapo wamemweleza kuwa asilimia kubwa tayari wameshajiandikisha.

Uchaguzi wa viongozi wa vijiji, mitaa na vitongoji katika utafanyika Novemba 27 mwaka huu.