RC Shinyanga anogesha siku ya wanawake duniani

SHINYANGA: KIKUNDI cha Mwanamke Chuma wilayani Kahama kimemkabidhi keki mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwa niaba ya wanawake wote katika kusherekea Siku ya Wanawake Duniani.

Mkuu wa Mkoa Mhita amekabidhiwa keki hiyo na Mkurugenzi wa kituo cha Redio Gold FM, Neema Mgheni ambaye anaratibu shughuli za mwanamke chuma katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanyika kata ya Uyogo Halmashauri ya Ushetu.

Mkuu wa Mkoa Mhita akipokea keki hiyo amesema amepata furaha kubwa kuona upendo wa dhati nakuwataka wanawake wote kuacha ubinafsi,kusemana na kuwa wamoja kujiinua kiuchumi.



