RC Shinyanga azima ndoa ya mwanafunzi

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, amefanikiwa kuzima ndoa ya mwanafunzi mwenye umri wa miaka 19, aliyechaguliwa kujiunga na kidato cha Tano katika moja ya shule za sekondari zilizopo Mkoa wa Tabora, mkazi wa Kijiji cha Mwawaza Wilaya ya Shinyanga.
Hatua hiyo imekuja baada ya wazazi wake kupokea mahari kwa kijana mwenye umri wa miaka 21 na kupanga siku ya kufunga ndoa ya kimila.
Mndeme akiwa na wadau wa msaada wa kisheria pamoja na kamati ya usalama Mkoa, jana walifika katika Kijiji cha Mwawaza wakiwa kwenye kampeni ya huduma ya msaada wa kisheria ya Mama Samia, baada ya kupata taarifa za siri na kufanikiwa kumuokoa binti huyo.
Mndeme alisema mwanafunzi huyo ambaye amemaliza shule ya sekondari Mwawaza mwaka jana na kuchaguliwa kuendelea na kidato cha tano mwaka huu, wazazi wake walikuwa wanataka kukatisha ndoto zake kwa kumuozesha bila ridhaa yake.
Mndeme alisema kitendo hicho hakiwezi kuvumiliwa ,kwani kinasababisha watoto wa kike washindwe kufikia malengo waliyojiwekea kutokana na tamaaza baadhi ya wazazi.
Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *