RC Shinyanga azindua mitambo kampuni ya madini

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme amezindua kuwasha kwa mitambo iliyozimwa baada ya kusitisha uzalishaji kwa kipindi cha miezi minane kwenye kampuni ya Williamson Diamond inayochimba madini ya almas iliyopo Mwadui wilayani Kishapu mkoani hapa.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la kuanza uzalishaji lilitolewa na Waziri wa Madini, Dotto Biteko baada ya kutembelea ujenzi wa bwawa tope jipya takribani wiki mbili zilizopita.

Mndeme alisema hayo jana wakati akiongoza zoezi la kuwashwa mitambo huku alitoa maelekezo kwa uongozi wa mgodi kuaanzisha bwawa lingine la dharura pindi inapotokea majanga mgodi usisimame kama ilivyokuwa na kuleta hasara.

“Kweli kampuni na serikali zimepata hasara kwa kipindi cha miezi nane siku nilipofika hapa kuona ujenzi wa bwawa unavyoendelea nikatoa maagizo mfanye kazi usiku na mchana haina tarehe moja mwezi Agost uzalishaji uanze lakini mmefanya kazi nzuri kabla ya tarehe hiyo uzalishaji umeanza hongereni sana”alisema Mndeme.

Mndeme alisema mmetimiza maagizo ya Waziri wa Madini na bwawa hili wamesema linauwezo wa kuhimili maji tope kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu.

Meneja wa mgodi huo, Mhandisi Ayoub Mwenda alisema kweli wamepata hasara kwani walikuwa wanazalisha kwa mwezi kareti 25000 hadi 30,000 na kareti moja katika soko bei yake ni Dolla 270.

“Katika kutoa mapato kwenye halmashauri na huduma kwenye jamii tulilizungumza na kusitisha kwa kipindi Cha miezi yote nane kwa kuwa uzalishaji unafanyika Tena huduma zitatolewa Kama kawaida” alisema Mwenda.

Kaimu mazingira mkoa wa Shinyanga Perfect Mbwambo alisema baada ya bwawa tope kupasuka mwaka Jana Hali ilikuwa sio nzuri kimazingira lakini sasa mazingira yako vizuri wanaupongeza uongozi wa Kampuni hiyo kutekeleza.

Mbunge wa jimbo la Kishapu, Boniface Butondo alisema mkuu wa mkoa amezindua rasmi na suala la maendeleo litakuja kwa Kasi kwani halmashauri itapata mapato na jamii kunufaika kwa CSR inayotolewa.

Habari Zifananazo

Back to top button