TABORA; Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dk.Batlida Buriani amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri ya Mkoa wa Tabora kununua viatilifu vya kuua mazalia ya mbu na viluilui kwa mapato yao ya ndani ili kupunguza idadi ya maambukizi ya ugonjwa wa Malaria.
Agizo hilo amelitoa wakati akiwapokea wabunge wanaounda mtandao wa wabunge wanaopambana na malaria na magonjwa yasiyopewa kipaumbele (TAPAMA) wakifanya ziara kuangalia huduma na maendeleo ya mapambano dhidi ya magonjwa hayo mkoani hapo.
Dk.Batilda ameelezea kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa malaria katika mkoa huo kilikuwa 11.7% kwa watoto kati ya umri wa miezi sita hadi 59 kwa mwaka 2017/2018 hivyo kuongezeka 23.4% hivyo kufanya mkoa huo kuwa na kiwango kikubwa cha maambukizi ya malaria katika jamii.
“Jiografia ya Mkoa wa Tabora kuwa na maeneo mengi yenye madimbwi ya maji yanayotumika katika maeneo mbalimbali ya makazi ya watu hasa kwenye kipindi hiki cha mvua zimechangia kuwa na kiwango cha juu cha maambukizi ya malaria “amesema Dk.Batilda
Pia,Dk.Batilda amesema kuwa imani potofu iliyojengeka katika jamii juu ya matumizi ya vyandarua vyenye dawa imeongeza hali ya maambukizi ya malaria hali iliyopelekea baadhi ya wananchi kutotumia vyandarua wanavyogaiwa katika vituo vya kutolea huduma za afya kwaajili ya matibabu badala ya waganga wa kienyeji.
Comments are closed.