REB yahimiza wakandarasi wazawa kujenga uwezo
BODI ya Nishati Vijijini(REB) imewahimiza wakandarasi wazawa kujenga uwezo, umahiri na weledi pindi wakabidhiapo miradi na Wakala wa Nishati Vijijini(REA).
Mwenyekiti wa bodi hiyo Meja Jenerali Jacob Kingu ametoa wito huo Dar es Salaam leo Agosti 24 wakati wa utoaji tuzo kwa wakandarasi waliofanya vizuri katika mradi wa PERI URBAN III.
SOMA: REA, EU wasaini umeme vijijini maeneo 426
Mradi huo umetekezeka kwa mikoa nane ambayo ni Tanga, Singida, Tabora, Kagera, Geita, Kigoma, Mtwara na Mbeya waliokabidhiwa Februari 2023.
Meja Jenerali Kingu amesema ili wakandarasi wazawa waweze kuwa washindani ni lazima wajipange huku akitoa rai kwa wakandarasi wanakabidhiwa miradi kumaliza kwa wakati.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa umeme vijijini Jones Olotu amesema mikoa hiyo ilichaguliwa katika mradi huo PERI URBAN III kutokana na mahitaji pamoja na maombi waliyoyapata.
Naye Mkurugenzi wa Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Hassan Saidy amesema wakandarasi wana wajibu wa kuleta vifaa vyenye ubora na kufanya kazi za ujenzi kwa kutumia weledi.
Makampuni yaliyomepewa miradi hiyo ni Dieynem Limited, Derm Group Limited, Central Electrical International Limited na Ok Electrical &Electronics Services Limited.