Refa wa kikongo kuamua fainali shirikisho
SHIRIKISHO la soka Afrika (CAF) limemtangaza mwamuzi mwenye beji ya FIFA, Jean-jacques Ndala (35) raia DR Congo kuwa pilato katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa fainali ya kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga dhidi USMA Alger Mei 28, 2023 Uwanja Mkapa, Dar-es-Salaam
Taarifa iliyotolewa jana na CAF imeeleza Ndala atasaidiwa na mwamuzi Zakhele Thusi kutoka Afrika Kusini na Olivier Safar kutoka DRC
Ndala anasifika kwa maamuzi yasiyo na mashaka ikiwemo mchezo wa kugombea nafasi ya kushiriki michuano ya Mataifa bingwa Afrika kati ya Ghana dhidi ya Angola Machi 23, 2023 mchezo uliomalizika kwa Ghana kushinda 1-0.