Rita yaagizwa vyeti vya kuzaliwa saa 48

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk Juma Homera amezindua mpango wa Wakala ya Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) wa utoaji wa vyeti vya kuzaliwa ndani ya saa 48 za kazi.

Dk Homera ameiagiza RITA kusimamia na kutekeleza mpango huo kwa weledi ili wananchi wapate huduma nyingine zinazotegemea cheti hicho. Akizindua mpango huo jijini Dar-es-salaam, Waziri Homera amesema uanzishaji wa mpango huo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyesisitiza vyeti vya kuzaliwa vipatikane ndani ya saa 48 za kazi.

Dk Homera amesema mchakato wa kupata cheti cha kuzaliwa utakuwa rahisi endapo waombaji watakuwa na viambatanisho ikiwemo barua ya serikali ya mtaa, taarifa za hospitali na vielelezo kutoka taasisi za dini ikiwemo misikiti na makanisa. Hatahivyo, ameipongeza taasisi hiyo kwa mafanikio waliyoyapata akisema hadi kufikia Novemba 25, mwaka huu wametoa vyeti vya kuzaliwa milioni 11.5. SOMA: Katibu Mkuu Dk Mwamba akutana na Mkurugenzi Afritac East

Amesema kwa mujibu wa takwimu za Rita hadi Novemba, mwaka huu Watanzania milioni 20 wamesajiliwa ikilinganishwa na Watanzania 205,000 waliokuwa wamesajiliwa mwaka 2004. Katika hatua nyingine, aliitaka Rita kuendelea kusimamia kwa ufanisi taasisi zote zilizo chini yake pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala ya uandishi na usimamizi wa mirathi, ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima katika jamii.

Kwa upande wake, Kabidhi Wasii Mkuu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa RITA Frank Kanyusi amesema mahitaji ya vyeti vya kuzaliwa ni makubwa na kwamba mpango huo mpya utasaidia kupunguza msongamano wa wananchi wanaosubiri huduma katika taasisi mbalimbali za umma. “Rita ndiyo taasisi ya kwanza kutoa utambulisho rasmi wa Mtanzania pale tu anapozaliwa na cheti hiko ni muhimu sana katika upatikanaji wa huduma nyingine kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini ikiwemo upatikakanaji wa hati ya kusafiria na mengineyo,” alisema.

Kanyusi amesema hadi Novemba 25, mwaka huu Rita imesajili vyeti vya ndoa zaidi ya milioni moja, vyeti vya vifo zaidi ya 12,000 na maboresho ya kiutawala na kidijiti. Naye mmoja wa wananchi aliyenufaika na mpango huo, Fatuma Saidi alisema alipata cheti cha kuzaliwa cha mtoto wake ndani ya saa 48 za kazi. “Nilitegemea kupata cheti ndani ya wiki mbili au tatu, lakini nilishangaa kuambiwa ndani ya saa 48 kuwa cheti changu kiko tayari,” alisema Fatuma.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. Google provides awesome remote work opportunities, allowing me to earn $2000-$3000 weekly with just 2-4 hours of daily work. It’s been a game-changer, offering flexibility and reliable income. If you’re seeking a genuine way to earn online, don’t miss this chance. Start today and transform your life!
    .
    More Details For Us →→ http://www.big.income9.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button