Katibu Mkuu Dk Mwamba akutana na Mkurugenzi Afritac East

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Taasisi ya Afritac East, iliyoko chini ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Clara Mira, kuhusu program ya kuongeza ujuzi na kuangalia maeneo mahususi ya kuongeza uwezo.

IMF inaendesha program ya kuongeza ujuzi katika nchi za Afrika, ikiwemo Tanzania, Rwanda, Uganda, Kenya, Eritrea na Malawi.
Mkutano huo umehudhuliwa pia na Mwakilishi Mkazi wa IMF, Sebastian Acevedo na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Sera, Wizara ya Fedha, Dk Remidius Ruhinduka.