Robo fainali za kibabe EURO2024 leo

MICHEZO miwili ya kukata na shoka ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya(EURO 2024) inapigwa leo viwanja tofauti huko Ujerumani.

Wenyeji Ujerumani itaikabili Hispania inayoonekana ya moto mwaka huu kwenye uwanja wa MHP uliopo jiji la Stuttgart.

Patashika nyingine itashuhudia Ureno ikimalizana na Ufaransa kwenye uwanja wa
Volkspark uliopo jiji la Hamburg.

Wachezaji wa kikosi cha Ujerumani wakiwa kwenye mazoezi kuelekea mchezo dhidi ya Hispania leo.(Picha:Germany Football Team )

Kwa hakika michezo hiyo miwili inasubiriwa kwa hamu na wapenda soka duniani kwani inazikutanisha timu zenye ubora wa hali ya juu wa mpira wa miguu.

Hispania na Ujerumani wamekutana takriban mara 25 katika mashindano rasmi na mechi za kirafiki.
Ujerumani ikishindi 9, Hispania mara 8 na zimetoka sare 8.

Katika mechi za Ureno na Ufaransa, zimekutana takriban mara 28 katika mashindano rasmi na mechi za kirafiki Ufaransa ikishindi 19, Ureno ushindi mara 7na sare 2.

Soma: http://Fainali za Ulaya 2024 zaanza leo

Zifuatazo ni takwimu za michezo kati ya Hispania na Ujerumani: katika mashindano makubwa na mechi za kirafiki:

Kombe la Dunia la FIFA

 • 1966: Ujerumani Magharibi 2-1 Hispania (Hatua ya Makundi)
 • 1982: Ujerumani Magharibi 2-1 Hispania (Hatua ya Makundi)
 • 1994: Ujerumani 1-1 Hispania (Hatua ya Makundi)
 • 2010: Hispania 1-0 Ujerumani (Nusu Fainali)

Mashindano ya Ulaya ya UEFA

 • 1984: Hispania 1-0 Ujerumani Magharibi (Hatua ya Makundi)
 • 1988: Ujerumani 2-0 Hispania (Hatua ya Makundi)
 • 2008: Hispania 1-0 Ujerumani (Fainali)
 • 2020: Hispania 6-0 Ujerumani (Hatua ya Makundi, UEFA Nations League)

UEFA Nations League

 • 2020: Ujerumani 1-1 Hispania (Hatua ya Makundi)
 • 2020: Hispania 6-0 Ujerumani (Hatua ya Makundi)

Mechi za Kirafiki

 • 1952: Hispania 2-2 Ujerumani Magharibi
 • 1958: Ujerumani Magharibi 2-0 Hispania
 • 1966: Ujerumani Magharibi 2-1 Hispania
 • 1971: Hispania 2-1 Ujerumani Magharibi
 • 1973: Hispania 2-2 Ujerumani Magharibi
 • 1974: Ujerumani Magharibi 2-1 Hispania
 • 1977: Hispania 1-1 Ujerumani Magharibi
 • 1980: Ujerumani Magharibi 2-2 Hispania
 • 1990: Hispania 2-0 Ujerumani
 • 1994: Ujerumani 1-1 Hispania
 • 2000: Ujerumani 4-1 Hispania
 • 2003: Hispania 3-1 Ujerumani
 • 2010: Hispania 0-1 Ujerumani
 • 2014: Hispania 0-1 Ujerumani
 • 2018: Ujerumani 1-1 Hispania

Nazo takwimu za michezo kati ya Ureno na Ufaransa ni kama ifuatavyo:

Kombe la Dunia la FIFA

 • 2006: Ufaransa 1-0 Ureno (Nusu Fainali)

Mashindano ya Ulaya ya UEFA

 • 1984: Ufaransa 3-2 Ureno (Nusu Fainali)
 • 2000: Ufaransa 2-1 Ureno (Nusu Fainali)
 • 2016: Ureno 1-0 Ufaransa (Fainali, muda wa ziada)
 • 2020: Ufaransa 2-2 Ureno (Hatua ya Makundi)

UEFA Nations League

 • 2020: Ufaransa 0-0 Ureno (Hatua ya Makundi)
 • 2020: Ureno 0-1 Ufaransa (Hatua ya Makundi)

Mechi za Kirafiki

 • 1926: Ureno 2-4 Ufaransa
 • 1945: Ureno 0-3 Ufaransa
 • 1953: Ureno 0-3 Ufaransa
 • 1959: Ureno 3-5 Ufaransa
 • 1975: Ureno 0-2 Ufaransa
 • 1978: Ufaransa 2-0 Ureno
 • 1983: Ufaransa 3-0 Ureno
 • 1996: Ureno 0-3 Ufaransa
 • 2001: Ureno 1-4 Ufaransa
 • 2011: Ureno 0-1 Ufaransa
 • 2014: Ureno 1-2 Ufaransa
 • 2015: Ureno 0-1 Ufaransa

Habari Zifananazo

Back to top button