Ruben Amorim kuiwahi Chelsea Old Trafford

Kocha Mkuu wa Sporting CP, Ruben Amorim.

TETESI za usajili wa soka zinasema Manchester United inatumaini kumpeleka Ruben Amorim Old Trafford kabla ya kipute cha Ligi Kuu England dhidi ya Chelsea Novemba 1, baada ya kuweka wazi nia yao kwa kocha huyo wa Sporting CP. (The Times)

Hata hivyo, Amorim amekiri hakuna uamuzi uliofikiwa kuhusu hatma yake na anatarajiwa kubaki akiinoa Sporting itakapoikabili Estrela katika mchezo wa Ligi Kuu Ureno, Novemba 1. (CNN – Portugal)

Beki wa Barcelona, Eric Garcia anahitajika Real Sociedad na Girona, huku klabu hiyo ikiwa na nia kufanya uhamisho kwa mkopo Januari, 2025. (Mundo Deportivo)

Advertisement

SOMA: Chelsea vs Man United mechi ya rekodi

Tottenham Hotspur inapanga kuimarisha safu yake ya ulinzi Januari 2025 na ipo sokoni kumsajili beki mpya. (Football Insider)

Chelsea inaweza kufanya mpango wa uhamisho wa Viktor Gyokeres wa Sporting CP, ambaye alikuwa katika rada za vilabu kadhaa vya Ulaya majira yaliyopita ya kiangazi.

Klabu hiyo inaweza kupata ushindani kutoka Arsenal, Liverpool na Manchester City ambazo pia zimeonesha nia kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Sweden. (Florian Plettenberg)

Newcastle United ‘The Magpies’ imeonesha nia kumsajili fowadi wa Brentford ‘The Bees’, Bryan Mbeumo, lakini inakabiliwa na ushindani kutoka Arsenal na Liverpool iwapo zinataka kumsajili mfungaji huyo ambaye yupo katika kiwango bora.

The Magpies inakabiliwa na masharti ya matumizi ya fedha huku The Bees ikimweka mchezaji huyo katika thamani ya pauni milioni 50. (Telegraph)