Rubi ya Afrika yavunja rekodi mauzo New York

MADINI aina ya Ruby kutoka Msumbiji yamevunja rekodi katika historia ya mnada wa madini ya vito wa New York, nchini Marekani kwa kuuzwa kwa donge nono la Paundi milioni 28, sawa na Dola za Marekani milioni 34.8 sawa na zaidi ya Sh bilioni 80.04 za Tanzania.
Madini hayo yenye karati 55.22, awali yalikuwa na uzito wa karati 101 mara baada ya kupatikana katika machimbo ya madini hayo mwaka jana nchini Msumbiji.
Madini hayo adimu yamepewa jina la “Estrela de Fura”, linalomaanisha “Nyota ya Fura” kwa Kireno, lililopewa jina la mgodi ambao lilipatikana.
Mkuu wa Mnada wa Sotheby’s, Quig Bruning jijini New York alisema alipoona jiwe hilo la Ruby kwa mara ya kwanza aliduwaa kwa kushangaa.
“Kwa ukubwa, rangi na upekee wake unaovutia ni nadra sana kupata madini ya vito kama hili,kwa kweli linastahili kuvunja rekodi ya mauzo kwa leo, kuanzia sasa vito hivi vinaungana katika orodha ya madini ya vito muhimu zaidi duniani,”alisema.
Mgodi wa Fura, Msumbiji uko katika wilaya ya Montepeuz katika Jimbo la Cabo Delgado eneo ambalo vikundi vya kigaidi walivamia na kufanya uharibifu.
Eneo hilo lina utajiri mkubwa wa rasilimali za madini ambazo havijatumika.
Mwaka 2009 hifadhi kubwa ya rubi iligunduliwa Kaskazini mwa Msumbiji na sasa nusu ya vito vyekundu duniani vinatoka huko.
Sotheby’s ilisema sehemu ya mapato ya mauzo ya Estrela de Fura inatengwa na Fura kuanzisha chuo cha kutoa mafunzo ya kiufundi katika fani za madini, uhandisi, useremala na kilimo.
Mining Census 2023
Watanzania mnakaribishwa kwenye SENSA ya Madini 2023 yenye lengo la kujua idadi ya migodi Tanzania, Idadi ya wachimbaji au watanzania wanaoshughulika na sekta ya Madini, Hali ya uchimbaji wa madini (zana zitumikazo kwa kila mgodi) na mapendekezo ya mbinu za kuboresha Sekta ya Madini.