Ruto ataka migogoro ya mipaka kutatuliwa

RAIS William Ruto wa Kenya ametoa wito kwa Rais wa Sudan, Salva Kiir kumaliza mzozo katika eneo la Upper Nile na Jonglei sambamba na kuelekeza juhudi zake katika kuimarisha huduma za kibinadamu.

Ruto alisema kuongezeka kwa uhasama katika maeneo hayo kunaweza kuharibu makubaliano ya amani yaliyofikiwa mwaka 2018.

“Hali ya kuongezeka kwa ukosefu wa usalama, ghasia, kufukuzana na migogoro ya kibinadamu inayoendelea katika maeneo hayo ni hatari kwa amani na utulivu wa Sudan Kusini na eneo lote la Afrika Mashariki kwa jumla,” alisema Dk Ruto.

Mapigano makali kati ya makundi yanayopingana huko Upper Nile na sehemu za majimbo ya Jonglei yamekuwa yakiendelea tangu katikati ya mwezi wa Agosti mwaka huu, na kusababisha raia wengi kuyahama makazi yao kutafuta maeneo yenye usalama ambapo wanawake na watoto ndiyo wanaoonekana kuathirika zaidi.

Katika taarifa aliyoitoa mwishoni mwa wiki Rais Ruto alisema mgawanyiko wa  kisisasa unaweza kunadhoofisha matumaini yoyote ya kuanza tena utekelezaji wa makubaliano ya amani yaliyohuishwa jambo ambalo si jema kwa ustawi wa Sudan na raida wake.

Aidha aliomba jumuiya ya kimataifa kuingilia kusuluhisha mgogoro huo ambao umedumu kwa takribani miezi mitano.

Wanaharakati, mashirika ya misaada na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo wamelaani ghasia hizo na kuitaka serikali ya kitaifa kupeleka vikosi vya usalama kudhibiti hali ya machafuko katika maeneo hayo.

Habari Zifananazo

Back to top button