Saada: Filamu fupi zinalipa wasanii kazi kwenu

MTAYARISHAJI  na muongozaji wa Filamu ya ‘Mwandishi’ inayoshikilia tuzo ya Kimataifa ya filamu bora fupi ya ZIFF 2023 Juma Saada ámesema filamu fupi ni fursa kubwa ambayo wasanii wengi nchini bado hawaijui.

Juma Saada anayeshikilia tuzo ya filamu bora fupi katika tuzo za filamu Tanzania za mwaka 2021 kupitia filamu ya ‘Mwandishi’ na tuzo ya muongozaji bora wa filamu nchini kupitia filamu ya ‘Nakupenda’ aliyoipata katika tuzo zilizotolewa mwaka 2022 amesema ametembea nchi nyingi ameona filamu fupi zinavyopendwa, zinatazamika kwa urahisi na uandaaji wake hauchukui muda mwingi.

“Mimi tangu nimeanza kuongoza filamu na kuandaa filamu fupi na ndizo zinazonilipa mno na kupitia hizo nimeitangaza sana nchi yangu kupitia mialiko mingi nayopata kutokana na filamu fupi ambazo pia zimeshinda tuzo mbalimbali ikiwemo filamu na uongozaji bora,

wanaosema hazilipi pole kwao mimi naingiza fedha kupitia hizi filamu fupi” anasema Juma.

Juma anafafanua kwamba wanachotakiwa wasanii, waigizaji na waongozaji wa filamu nchini wafanye, waache kufanya kazi za sanaa kwa mdomo wafanye kwa vitendo na pia wawekeze katika uandaaji wake na waachane na fikra ya kwamba haziuzi.

”Soko ni kubwa mno la filamu fupi kinachotakiwa wafanye vitendo badala ya kulalamika kwamba haziuzi wakati hujafanya hata moja, au uliyofanya uandaaji wake mbovu haufai kwenye ushindani wa soko la kuonyeshwa kwenye majumba ya sinema, sanaa imebadilika ukiifanya kama kazi itakulipa ila ukiifanya mdomoni itakuacha katika majuto ya lawama,” ameeleza Juma Saada.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Angila
Angila
15 days ago

Making every month extra dollars by doing an easy job Online. Last month i have earned and received $18539 from this home based job just by giving this only mine 2 hrs a day. Easy to do work even a child can get this and start making money Online. Get this today by follow instructions
.
.
.
On This Website……………..> > http://remarkableincome09.blogspot.com

Last edited 15 days ago by Angila
Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x