UWANJA wa ndege wa Bukoba umefunguliwa tena baada ya kufungwa kwa muda kufuatia ajali ya ndege ya Precision Air iliyotokea Novemba 6 mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 19.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Albert Chalamila amewaambia waandishi wa habari kuwa “uwanja wa ndege wa Bukoba umefunguliwa rasmi na tayari kutoka saa kumi na mbili leo asubuhi safari za ndege zimeruhusiwa kuanza.”
“Ajali za ndege hazitokei mara kwa mara kama ilivyo kwa gari au kifaa chochote, linapotokea jambo kama hili basi huwa ni mara chache sana tena ikiwezekana kwa miaka mingi mno kwahiyo niwatoe wasiwasi wananchi wote, hata mimi mwenyewe leo baada ya safari za ndege kuanza rasmi katika uwanja huu nitapambana kuelekea mahali ambapo sitaki kuwaambia naenda wapi.”