Sagini apongeza hospitali Mbeya kwa ubunifu

MBEYA; Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Jumanne Sagini, ameipongeza Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya kwa kuboresha huduma za afya, kuimarisha ubunifu wa teknolojia na kuzingatia utu katika kuhudumia wagonjwa.

Sagini ametoa pongezi hizo wakati wa ziara yake hospitalini hapo, ambapo alisisitiza kuwa huruma, upendo na namna watumishi wa afya wanavyowapokea wagonjwa ni sehemu muhimu ya matibabu, kwani hujenga matumaini ya kupona hata kabla ya kuanza kutumia dawa.
Pia amepongeza uongozi wa hospitali hiyo kwa kuhamasisha ubunifu wa ndani unaosaidia kurahisisha utoaji wa huduma za afya kwa wateja wanaofika.



