Said Mtanda aagiza malipo ya fidia wakazi Mwanza

MWANZA: MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, ameitaka Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza kulipa fidia ya Sh milioni 285 kwa wakazi wa mitaa ya Nyafula, Igalagala, Ilelako,Sangabuye na Lugeye iliopo katika kata ya Sangabuye.

Deni hilo limetokana na uuzaji wa viwanja vya wananchi kupitia mradi wa viwanja vya Nyafula kata ya Sangabuye ulioratibiwa na Manispaa ya Ilemela mwaka 2022.

Mtanda ametoa agizo hilo Mei 12 wakati wa usikilizaji wa kero za wananchi katika viwanja vya Nyafula..

Mtanda ametoa pole kwa wananchi zaidi ya 50 wanaodai fidia za mwaka 2022 zinazohusiana na mradi wa viwanja vya Ilemela pamoja na wananchi waliopisha maeneo ya machinjio.

“Nasisitiza maniapaa ya Ilemela  kuhakikisha madeni yote ya fidia yanalipwa ndani ya miezi mitatu kuanzia mwezi huu na  wananchi wa Sangabuye wanapaswa kulipwa fidia zao kwa wakati ili kuepusha migogoro ya ardhi na kuharakisha maendeleo ya miradi,” amesema

Vile vile Mtanda amesema kuwa mikutano ya kushughulikia suala la kero za wananchi itaendelea kufanyika ili kuhakikisha wananchi wote wanaostahili wanapatiwa haki zao.

Amesisitiza kuwa hakuna mradi wowote utakaoendelea bila wananchi kulipwa fidia zao kwanza.

Naye Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Goodluck Lukandiza alikiri deni la Halmashuri yao ni Sh milioni 285.

“Kwa sasa, deni lote la fidia ambalo bado halijalipwa katika Mradi wa Viwanja vya Nyafula ni Shilingi 285 likijumuisha uthamini wa marudio katika mitaa ya Sangabuye, Lugeye, Ilekako, Igalagala pamoja na uthamini wa Mlima Lugeye,” amesema.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button