Salome Makamba aipongeza PBPA utendaji kazi bora

DAR ES SALAAM: Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba ameupongeza Wakala ya Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) kwa utendaji kazi mzuri katika kuhakikisha nchi inakuwa na akiba ya mafuta ya kutosha.

Salome Makamba ameyasema hayo alipozungumza na Menejimenti ya PBPA leo Desemba 6, 2025 jijini Dar es Salaam.

“Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya lakini hakikisheni mnatoa elimu kwa Watanzania kuhusu majukumu yenu na kazi zenu,” amesema Salome.

Aidha, ametumia nafasi hiyo kuitaka PBPA kuwawezesha Watanzania wazawa kuingia kwenye biashara ya mafuta na kufanya kazi kwa ushirikiano.

“Lazima tupate wawekezaji wa Tanzania, tuwawezeshe waingie kwenye hii biashara,” amesisitiza Salome.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala ya Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Erasto Simon amesema wakala hiyo imefanikiwa kuhakikisha kunakuwa na akiba ya mafuta ya kutosha, uwepo wa takwimu sahihi za kiasi cha mafuta pamoja na kuiwezesha Serikali kupanga ukusanyaji wa mapato.

“Mfumo wa Bulk Procurement System (BPS) umesaidia hata nchi za jirani kuagiza mafuta kwa karibia asilimia 95 sambamba na kudhibiti ubora wa bidhaa za mafuta yanayoingia nchini.

Amefafanua kuwa nchi za jirani kama Malawi, Zambia, Uganda, Rwanda, Zimbabwe na Namibia wanaendelea kutembelea Tanzania na kujifunza kuhusu namna bora ya uagizaji mafuta katika nchi zao.

Amesema PBPA imefanikiwa kuratibu uagizaji wa mafuta kwa ufanisi mkubwa kutokana na uwazi uliopo katika mchakato mzima wa uagizaji mafuta.

Lengo la ziara ya Makamba katika ofisi za PBPA ni kujifunza kuhusu majukumu ya PBPA pamoja na kujitambulisha mara baada ya kuteuliwa na Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Nishati.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. Single Mom Reveals How She Earns $89k/Yr Working 10 Hrs/Week From Home. Tired of paycheck-to-paycheck living? Meet Kelly from New York—a regular mom who cracked the code to recession-proof income without selling a thing! Now,Big thanks …
    .
    Here is I started____________________ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button