Samia aileta dunia Dar

RAIS Samia Suluhu Hassan anaungana na wakuu wa nchi 24 Afrika, makamu wa rais, mawaziri wakuu na manaibu mawaziri wakuu 10 katika Mkutano wa Nishati Afrika (Mission 300) unaoanza leo jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo pia unajumuisha mawaziri wa nishati na uchumi 60 pamoja na wadau wa maendeleo wakiwemo Rais wa Benki ya Dunia, Ajay Banga na Rais wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Dk Akinwumi Adesina na washiriki wengine zaidi ya 2,600.

Kauli mbiu ya mkutano huo ni ‘Kuharakisha Upa[1]tikanaji wa Nishati Afrika’ umelenga kuangazia dhana nzima ya upatikanaji wa umeme kwa wote hususani katika nyakati ambazo viongozi wa Afrika wanasisitiza matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Advertisement

Mkutano huo wa kihis[1]toria unalenga kuimarisha juhudi za pamoja kuhakiki[1]sha umeme unawafikia watu milioni 300 barani Afrika katika kipindi cha miaka mitano kuanzia sasa ili kuongeza idadi ya wanaopata nishati hiyo Afrika iwe ya uhakika, nafuu na endelevu. uhakika, nafuu na endelevu. Kwa mujibu wa taarifa za upatikanaji wa umeme Afrika, zaidi ya watu milioni 685 wanaishi bila umemE.

Viongozi waliowasili nchini tayari ni Rais wa Sierra Leone, Julius Maada Bio, Rais wa AfDB, Dk Adesina, Rais wa Benki ya Dunia, Banga, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Sao Tome na Principe, Patrice Trovoada, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Namibia, John Mutorwa, Rais wa Benki ya Miundombinu na Uwekezaji ya Asia, Liqun Jin na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Amina Mohamed.

Wengine waliotara[1]jiwa kuwasili jana jioni na baadaye usiku ni pamoja na Waziri Mkuu wa Ivory Coast na Waziri Mkuu wa Uganda, Makamu Waziri Mkuu na Waziri wa Ujenzi na Usafirishaji wa Namibia na viongozi wengine wanaowasili kulingana na ratiba.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, wakuu wa nchi wengine wanaotarajiwa kuwasili nchini leo ni pamoja na Mfalme wa Lesotho, Rais wa Comoro, Mwenyekiti wa Baraza la Serikali ya Libya, Rais wa Guinea Bissau, Botswana, Malawi, Bu[1]rundi, Mauritania, Ghana na Ethiopia. Pia, Waziri wa umeme na nishati wa Afrika Kusini, Naibu Waziri Mkuu wa Eswatini, Makamu wa Rais wa Gambia, Makamu wa Rais wa Benin.

Wengine wanaotarajiwa ni kutoka Nigeria, Gabon, Kenya, Liberia, Algeria, Sudan, Zambia, Somalia, Kongo Brazaville, Djibouti na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Aidha, wadau wengine 47 wa AfDB wanatarajiwa kushiriki mkutano huu na washirika wakubwa 25 wa Benki ya Dunia na watano kutoka Taasisi ya Rockfeller.

Leo ikiwa ni siku ya kwanza ya mkutano mawaziri wa sekta husika wanakutana kujadiliana na wataidhinisha makubaliano na washirika wenza wa maendeleo ya sekta binafsi na kuangalia maeneo wanayoweza kuunga mkono malengo ya Mission 300. Kesho, mkutano huo utahitimishwa na vikao vya wakuu wa nchi watakaoele[1]zana maono yao katika ukuaji wa sekta ya nishati na ushirikiano wa kikanda na hatimae wataridhia Azimio la Dar es Salaam kuhusu Nishati.

Aidha, kutasainiwa awamu ya kwanza ya Mi[1]pango Mahususi ya Kitaifa ya Nishati kwa kipindi cha 2025-2030 ambapo nchi 14 za Afrika zitahusika. Nchi hizo ni Tanzania, Burkina Faso, Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Niger, Msumbiji, Liberia, Madagascar, Malawi, Chad, Nigeria, Ivory Coast, Mauritania na Mali. Mkutano huo unaratibiwa na Benki ya Dunia, AfDB, Kamisheni ya Umoja wa Afrika na Tanzania.

Akizungumzia maan[1]dalizi ya mkutano huo juzi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Kombo alisema baada ya mkutano huo, Rais Samia Suluhu Hassan atafanya mazungumzo na baadhi ya wakuu wa nchi kuhusu mambo mbalimbali baina ya mataifa yao. Pia, wageni hao wanatarajia kutembe[1]lea vivutio vya utalii baada ya mkutano ambapo baadhi watakwenda katika hifadhi za taifa za wanyama na wengine watatembelea Zanzibar.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *