Samia asherehekea ‘birthday’ na watoto yatima

Samia asherehekea ‘birthday’ na watoto yatima

RAIS Samia Suluhu Hassan amesherehekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa leo  Januari 27, 2023, kwa kutoa vitu mbalimbali katika vituo saba  vya watoto yatima.

Vitu hivyo vimekabidhiwa mapema leo na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ambaye piani Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega, ambaye alimwakilisha Rais Samia, ambapo alikabidhi vitu mbalimbali na fedha taslimu

Tukio hilo limefanyika katika Kituo cha Children home Msimbazi cha Ilala jijini Dar es Salaam, pia alikabidhi zawadi hizo kwa Kituo cha Watoto Mburahati.

Advertisement

Katika tukio hilo, pia alitembelea na kujulia hali watoto hao wanaolelewa kituo hicho cha Msimbazi.

Baadhi ya vitu vilivyokabidhiwa ni pamoja na unga, Sabuni, sukari, maziwa,mafuta na vingine vingi.

Vituo vingine ambavyo vimepelekewa zawadi hizo ni  vituo vya Tuangoma, Mbagala, Mbweni, Mwasonga na Sinza