Samia asisitiza maadili bora kwa watoto

DAR ES SALAAM :RAIS Samia Suluhu Hassan ameisihi jamii kuhakikisha inawapatia malezi na maadili bora watoto.

Rais Samia amesema hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati akisherehekea Siku ya Mtoto wa Afrika na wajukuu zake, ambapo siku hiyo huadhimishwa Juni 16 ya kila mwaka.

Amesisitiza umuhimu wa Serikali, familia na jamii kushirikiana kuhakikisha watoto wanapata malezi bora yenye maadili mema, na kuhakikisha usalama wa mtoto ni jukumu la jamii nzima na siyo mzazi tu, vilevile kuwapatia elimu na historia za kuwahimiza uzalendo kwa nchi yao tangu wakiwa wadogo.

Habari Zifananazo

Back to top button