Samia ataka Uzalendo Sekta ya madini
DODOMA: Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inaendelea na mikakati ya kuiboresha sekta ya madini ikiwa ni pamoja na kuwafanya wachimbaji madini kunufaika kupitia sekta hiyo ndio maana serikali imeendelea kuthamini mchango wao.
Samia amesema katika kutekeleza hilo Serikali imewanunulia leseni wachimbaji wadogo 300 huku ikiendelea kuweka mazingira rafiki zaidi kwa wadau wa sekta hiyo.
Pia amewataka wafanyabiashara katika sekta hiyo kuachana na vitendo visivyofaa ikiwemo utoroshaji wa madini huku akiwasisitiza kuwa wazalendo ili kupata maendeleo yanayolengwa.
Rais Samia ameyasema hayo leo na Oktoba 21, 2023 mkoani Dodoma katika uzinduzi wa mitambo ya kuchorongea madini kwa wachimbaji wadogo wa Shirika la Madini la Taifa (Stamico).