Samia atoa pole kifo cha Membe

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje ya Nchi, Bernad Membe alilitumikia Taifa kwa weledi kipindi cha uhai wake.
“Kwa zaidi ya miaka 40, ndugu Membe alikuwa mtumishi mahiri wa umma, mwanadiplomasia, Mbunge na Waziri aliyeitumikia nchi yetu kwa weledi. Pole kwa familia, ndugu, jamaa & marafiki. Mungu amweke mahali pema. Amina,” ameandika Rais Samia kupitia ukurasa wake wa ‘Twitter’.

Habari Zifananazo

Back to top button