Samia atoa pole waliokufa migodini Simiyu

HABARI: Rais Samia Suluhu Hassan ametoa pole kwa familia za watu 21 waliokufa baada ya kufunikwa katika mgodi wa Ng’alita, Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu.

Rais Samia ametoa pole leo Januari 14, 2024 kwenye mitandao yake ya kijamii.

Kiongozi huyo wa nchi amesema: Natuma salamu za pole kwa ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza jamaa zao katika ajali hii,”

“Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vikishirikiana na uongozi wa mkoa vinaendelea na juhudi za kutafuta miili mingine ambayo bado imekwama ndani ya kifusi.”

Imeelezwa tukio hilo limetokea Januari 13, 2024 saa kumi na moja alfajiri.

Habari Zifananazo

Back to top button