Samia atuma salamu za rambirambi kifo cha Pele

Samia atuma salamu za rambirambi kifo cha Pele

Rais wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa Brazil, Jair Bolsonaro kufuatiwa kuondokewa na nguli wa soka Edson Arantes do Nascimento ‘Pele’ aliyefariki jana nchini Brazil.

“Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mwanasoka wa Karne kutoka Brazil “Pelé”. Mchango wake katika soka Duniani utakumbukwa daima. Pole kwa Rais wa Brazi Jair Bolsonaro, familia & mashabiki wote wa soka. Mungu amweke mahali pema peponi, Amina.” ameandika Rais Samia.

Pele alifanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye utumbo wake mnamo Septemba 2021 katika Hospitali ya Albert Einstein mjini Sao Paulo, baada ya uvimbe huo kugunduliwa katika vipimo vya kawaida.Alirejeshwa hospitalini mwishoni mwa Novemba 2022.

Advertisement

Binti yake Kely Nascimento amewafahamisha mashabiki kuhusu hali ya babake kwa taarifa za mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii kutoka hospitalini.

Siku ya Alhamisi alichapisha picha ya kile kilichoonekana kuwa mikono ya familia ya Pele kwenye mwili wake hospitalini na kuandika: “Kila kitu tulicho ni shukrani kwako. Tunakupenda sana. Pumzika kwa amani.”