Samia kutoa Sh Mil 5 kila goli Simba, Yanga CAF

#BreakingNews: RAIS Samia Suluhu Hassan, ameahidi kutoa Sh milioni 5 kwa kila goli litakalofungwa na timu za Simba na Yanga wakati wa michezo inayoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), ngazi ya klabu hatua ya makundi wikiendi hii, Msemaji Mkuu wa Serikali @MsigwaGerson amewaeleza Wahariri jijini Dar es Salaam.
Simba itakutana na vinara wa Kundi C, Raja Casablanca katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika Jumamosi wiki hii, wakati siku inayofuataYanga itacheza na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) katika Kombe la Shirikisho.
#HabarileoUPDATES

Habari Zifananazo

Back to top button