GHANA : RAIS wa Ghana Nana Akufo-Addo anakabiliwa na mzozo mkubwa mitandaoni ya kuzindua sanamu lake lililopewa jina la safari ya shukrani.
Unaambiwa sanamu hilo linasifiwa kwa jinsi lilivyosimikwa kwa heshima na kumuonyesha Rais Nana Akufo Addo akiwa amesimama.
Lakini Waghana wengi nchini humo wamelidhihaki sanamu hilo na kuitafsiri sanamu hilo ni njia ya kujitukuza.
Wananchi wa Ghana wamesema Rais Akufo-Addo hana sababu ya kutumia sanamu hilo kujisifu wakati ahadi zake kwa wananchi hajazitekeleza. SOMA: Makamu wa rais Ghana kugombea urais
“Watu wa Ukanda wa Magharibi wanastahili kuona jambo bora zaidi ya maonyesho ya kujionyesha ,” Mbunge wa upinzani Emmanuel Armah Kofi-Buah alichapisha kwenye mtandao wake wa X.
Akufo-Addo, ambaye atang’atuka madarakani Januari mwakani baada ya mihula miwili madarakani, amejigamba kuwa ametimiza asilimia 80 ya ahadi zake kwa Wananchi.