Saudia, Urusi kupunguza uzalishaji mafuta

LICHA ya changamoto ya upatikanaji na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia, Saudia Arabia na Urusi zimekubaliana kupunguza uzalishaji wa nishati hiyo kwa miezi mitatu hadi Disemba mwaka huu.

Bei ya mafuta ilipanda zaidi ya asilimia 1 jana baada ya mataifa hayo kutangaza nyongeza mpya ya upunguzaji wa usambazaji wa hiari, na kuongeza punguzo la jumla la mapipa milioni 1.3 kwa siku (bpd).

Hatua hiyo imefanya sasa bei ya mafuta kupanda kufikia zaidi ya Dola 90 sawa Sh 220,000 kwa pipa ikiwa ni kwa mara ya kwanza tangu Novemba 2022.

Hatua za Saudi Arabia na Urusi zinaimarisha juhudi za muungano unaojulikana kama OPEC+ unaojumuisha wanachama wa Shirika la Nchi Zinazouza Petroli na wazalishaji wengine kuunga mkono bei ya mafuta kwa kukubali kupunguzwa kwa uzalishaji.

Chanzo rasmi kutoka Wizara ya Nishati ya Saudia kililiambia Shirika la Habari la Serikali SPA kwamba hatua hiyo itaongeza upunguzaji wake wa uzalishaji wa mapipa milioni 1 kwa siku hadi mwisho wa Desemba.
Uamuzi huo “utakaguliwa kila mwezi ili kuzingatia kuongeza upunguzaji au kuongeza uzalishaji,” kiliongeza chanzo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button