Sekondari Nyaishozi mfano wa kuigwa ulimaji kahawa Kagera

NYAISHOZI Sekondari ni mfano mzuri wa juhudi za wakulima wa kahawa katika Wilaya za Karagwe na Kyerwa  mkoani Kagera kutafuta mabadiliko chanya katika jamii zao kupitia elimu.

Shule hii inayomilikiwa na Chama Kikuu cha Ushirika wa Kahawa (KDCU), ilianzishwa mwaka 1990 kwa lengo la kutoa elimu kwa watoto wa wakulima na kuleta mabadiliko katika kilimo cha kahawa, ili kijenge jamii yenye tija.

Advertisement

Mkuu wa shule hiyo,  Audax Gereon amesema lengo  lilikuwa ni kuwawezesha wakulima na familia zao kufikia maendeleo ya kijamii na kiuchumi kupitia elimu bora wanayopata watoto wao wanaosoma katika shule hiyo na kumaliza elimu ya chini hadi kufikia chuo kikuu.

Anasema kutokana na  shule hii kufanya vizuri hivi karibuni kumekuwa na mwitikio mkubwa kutoka kwa wakulima wa kahawa, ambao sasa wanapeleka watoto wao katika shule hii jambo ambalo limeleta Hamasa kubwa  kww shule hiyo kuanzisha mchepuo wa sayansi.

Anasema shule hiyo  mwaka 2024 imeshika nafasi ya 7 kitaifa kwa matokeo ya kidato cha sita baada ya wanafunzi 80 wote kupata Daraja la kwanza huku matokeo ya kidato cha nne  wanafunzi 141 walipata Daraja la kwanza.

“Wakulima hawa wa kahawa wameonyesha hamu kubwa ya kupata elimu bora kwa watoto wao, huku wakitambua kuwa elimu ni ufunguo wa mabadiliko katika familia na jamii zao na sisi uongozi wa shule tumeboresha miundo mbinu ya shule kwa kuweka ulinzi wa camera Kila eneo ,uzio, maji ya kutosha   na  bila kusahau SoMo la kilimo cha kahawa ambalo linaongoza wanafunzi kufundisha jamii zao wawapo likizo, “amesema  Greon.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karagwe Wales Mashanda amesema imekuwa fahari kuona wakulima kutoka wilaya zilizoanzisha shule hiyo wanapeleka watoto wao katika shule na kuona watoto hao wanakua katika ustawi mzuri huku kipaumbele kikubwa kikiwa ni watoto hao kuleta mabadiliko katika mashamba ya kahawa kupitia elimu wanayoipata.

Mmoja wa wazazi  Gozbeth Gabriel anasema Nyaishozi Sekondari inachukua watoto kutoka familia zote, lakini  wao kama wakulima wanajivunia  kuona watoto wa wakulima wa kahawa wanapata Elimu  ambapo wanaweza kujiunga na shule hii bila kulipa ada kubwa, badala yake, wazazi wanakata kiasi kidogo cha pesa kutokana na mauzo ya kahawa wanayozalisha.

Anasema huu ni mfumo wa kipekee unaoonyesha jinsi wakulima wanavyothamini elimu na kuweza kutoa fursa kwa watoto wao kupitia kilimo chao cha kahawa na jinsi waanzilishi wa shule hiyo wanavyojivunia kukomboa kizazi chao kupitia elimu.

2 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *