Sekta binafsi EA yajadili viwango kibiashara

JUMUIYA ya wafanyabiashara imeshauriwa kutumia shirika la kikanda la Afrika Mashariki la sekta binafsi kuibua masuala muhimu kuhusiana na uwianishaji wa viwango vinavyohitajika katika eneo hilo ili kurahisisha ufanyaji biashara.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC), John Kalisa alisema hayo katika taarifa iliyosomwa na Meneja wa Sera na Viwanda kutoka EABC, Frank Dafa katika mkutano wa kikanda sekta binafsi kujadili kuhusu viwango vya biashara.

Mkutano huo ulifanyika Alhamis Dar es Salaam na kukutanisha wadau mbalimbali wa sekta binafsi kutoka nchi za kikanda kwa kushirikiana na Taasisi ya Trade Mark East Africa (TMEA).

Dafa alisema anatamani kuona sekta binafsi na ya umma ikishiriki katika mazungumzo yenye maana na kushiriki kikamilifu katika ukuzaji wa viwango vya Afrika Mashariki viendeshwe na mahitaji badala ya mahitaji ya udhibiti.

Alisema baada ya kutambua changamoto katika eneo la viwango vya biashara, EABC imeanzisha mpango wa uhamasishaji wa kikanda kwa sekta teule unaotetewa kwa ajili ya mapitio ya sheria na kushiriki katika ukuzaji viwango katika kanda.

Alisema kwa kuzingatia mafanikio makubwa yaliyopatikana katika uwianishaji wa viwango vya Jumuiya ya Afrika Mashariki, bado kuna changamoto ambazo ni pamoja na kupitishwa na kuoanisha viwango, viwango endelevu katika vikwazo vya biashara visivyokuwa vya kiushuru (NTBs) na kasi ndogo ya kukamilisha muswada wa SACA.

Alisema ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) umepata mafanikio makubwa katika uwianishaji wa viwango  vya biashara.

Mwakilishi kutoka TMEA, Elibariki Shammy alisema ukanda huo unatumia viwango visivyostahili kwenye ushindani wa biashara ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki.

 

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button