Sekta ya utalii yathamini afya kupitia pato lake

Wizara ya Maliasili na Utalii imeeleza kuwa inathamini afya ya mama na mtoto kupitia mapato ya utalii yanayotokana na maeneo yaliyohifadhiwa ambapo kwa sasa inachangia asilimia 17 ya Pato la Taifa.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mtoto Njiti Duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Robanda Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amesema wizara hiyo mekua ikishiriki moja kwa moja katika kuchangia maendeleo ya afya ya mtoto.

Maadhimisho hayo yaliyoambatana na matukio mbalimbali ya wadau kuchangia fedha na vifaa kwa ajili ya kuhudumia watoto njiti yakiongozwa na Taasisi ya Doris Mollel Foundation (DMF).

Masanja ameipongeza taasisi hiyo kuandaa matukio mbalimbali likiwemo la kurusha balloon katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa lengo la kuitangazia dunia kuwa inamtambua na kumthamini mtoto njiti na kuonesha kwamba thamani hiyo inaweza kuonekana kupitia mchango mkubwa wa Sekta ya Utalii hapa nchini.

“Nikiwa kama Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza, naishukuru taasisi ya Doris Mollel Foundation kwa kutoa vifaa vitakavyoenda kuokoa maisha ya watoto njiti Kanda ya ziwa.” amesema Masanja.

Aidha, amemshukuru Rais. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa mchango wa fedha taslimu kutoka kwenye mshahara wake kiasi cha shilingi milioni 20 itakayotumika kujenga chumba maalum cha kumhudumia mtoto njiti, na pia kwa kutoa vifaa vya kuhudumia watoto njiti vyenye thamani ya shilingi milioni 50.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button