Sensa ya wanyamapori yazinduliwa Morogoro

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Dk Pindi Chana amezindua rasmi zoezi la Sensa ya Wanyamapori lengo ikiwa ni kuhesabu wanyamapori nchi nzima kwa uhifadhi wa rasilimali za wanyamapori, misitu na kuendeleza utalii.

Uzinduzi huo utakaogharimu Sh milioni 560 katika mfumo wa Ikolojia ya Nyerere – Selous – Mikumi yenye kilomita za mraba 104,143 umefanyika katika eneo la Matambwe Hifadhi ya Taifa ya Nyerere leo mkoani Morogoro.

“Zoezi hili linathibitisha jitihada za serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk Samia Suluhu Hassan katika uhifadhi wa rasilimali za wanyamapori na misitu nchini na kuendeleza utalii,” Dk Chana amesema.

Advertisement

SOMA: Hii hapa nembo ya asali Tanzania

Amesema sensa hiyo katika ikolojia ya Nyerere – Selous- Mikumi  ni sensa ya 17 tangu kuanza kuhesabu wanyamapori katika eneo hilo na litafanyika kuanzia Oktoba,5 hadi Novemba 14, 2024.

Akizungumzia mchango wa  sekta hiyo, Dk Chana amesema kupitia uhifadhi sekta ya maliasili na utalii inachangia asilimia 21% ya pato la taifa, asilimia 25% ya fedha za kigeni, kuzalisha ajira takribani Sh milioni 1.6 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja.

Amefafanua kuwa sensa hiyo itahusisha maeneo ya Hifadhi za Taifa za Nyerere, Mikumi, Mapori ya Akiba, Selous, Lukwika-Lumesule, Liparamba na Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori za Chingolie, Iluma , Jukumu, Kisungule, Kimbanda, Mbaran’gandu, Nalika-Tunduru, Ngarambe-Tapika, Liwale na Maeneo ya wazi yanayozunguka mfumo wa Ikolojia hiyo.

SOMA: Dk Chana aonya wawekezaji wasioendeleza maeneo

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), Dk Eblate Mjingo amesema sensa ya wanyamapori huonesha viashiria ambavyo ni changamoto kwa wanyamapori na huisaidia Serikali kutenga rasilimali kwa ufanisi kukabiliana na ujangili, kuendeleza na kukuza utalii pamoja na kupunguza migongano baina ya binadamu na wanyamapori.

Zoezi hilo linafanyika kwa ushirikiano wa Taasisi zilizo  chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii zikiwemo Tanapa na Tawa chini ya uratibu wa Tawiri.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by HABARILEO (@habarileo_tz)