‘Serikali iweke nguvu madhara ya teknolojia kwa watoto’
DODOMA: MBUNGE wa Jimbo la Buchosa, Eric Shigongo ameishauri Serikali kuwekeza katika kuishauri jamii madhara ya matumizi kupita kiasi ya teknolojia kwa watoto.
Akizungumza leo bungeni jijini Dodoma, Shigongo amesema eneo la pili ambalo serikali inatakiwa kuweka nguvu ni kudhibiti matumizi ya simu shuleni.
Shigongo ameshauri wazazi kupunguza tabia za watoto wao kuwahusisha zaidi na masuala ya teknolojia, na matumizi ya simu kwa ajili ya kulinda kizazi kilichopo na baadaye.
“Sisi kama Watanzania tuwalinde watoto wetu na mambo haya tusiwaweke sana watoto wetu kwenye mitandao hatutakuwa na Watanzania bora siku za kesho,” amesema Shigongo.
Shigongo amesema ni bora kuwaruhusu watoto kutumia teknolojia wakati wa kufanya kazi za shule wakiwa nyumbani, lakini pia kuepuka kuwapa watoto simu katika kipindi ambacho hawastahili.