Serikali kuboresha mazingira ya uwekezaji
WAZIRI wa Fedha, Mwigulu Lameck Nchemba ameihakikishia Jumuiya ya Kimataifa na Watanzania kwa ujumla kwamba serikali inaendelea kuweka na kuboresha mazingira ya uwekezaji ikiwemo kuboresha mifumo ya kodi.
Kiongozi huyo ametoa kauli hiyo leo Agosti 21, 2024 alipowasili ofisi ndogo za Wizara ya Fedha zilizopo mkoani Dar es Salaam kwa lengo la kuagana na Balozi wa Uswisi, Didier Chassot aliyemaliza muda wake nchini.
Akizungumza na balozi huyo, Dk Mwigulu amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameunda timu ya wataalamu kupitia na kuja na mapendekezo yatakayosaidia kuboresha mifumo ya kodi ili kuvutia zaidi biashara na uwekezaji nchini.
SOMA: Bajeti ya tril 49/- kuleta nafuu
Amefafanua kuwa serikali imechukua hatua kadhaa za uboreshaji kielektroniki ya ukusanyaji kodi inayosaidia kukusanya mapato yake kwa ufanisi na kuondoa usumbufu kwa walipa kodi.
📍Geita
VIDEO:
Waziri wa Fedha Dkt Mwigulu Nchemba alipomuwakilisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe . Dkt Dotto Biteko katika Jubilei ya miaka 25 ya Updre ya Askofu Flavian Matindi Kassala,iliyofanyika katika kanisa kuu la bikira Maria Malkia wa Amani,mkoani Geita… pic.twitter.com/gsQrv2MnUj
— Haki Ngowi (@Hakingowi) August 14, 2024
“Lengo letu ni kuhakikisha kuwa idadi ya walipakodi inaongezeka hatua itakayosaidia pia kuiwezesha serikali kupunguza viwango vya kodi ya ongezeko la thamani siku za usoni kwa sababu walipakodi watakuwa wengi,” alisema waziri Nchimbi.
Kwa upande wake Balozi wa Uswisi, Didier Chassot aliyemaliza muda wake hapa nchini aliipongeza serikali kwa uamuzi huo wa kupitia mifumo ya kodi na kwamba anaamini mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania watapata pia nafasi ya kuzungumza na kujadiliana na serikali kuhusu masuala hayo kama walivyoomba.
SOMA: Mwenendo wa shilingi ni tulivu -Mwigulu
Kwa kuongezea balozi huyo alisema kuwa Uswisi inaandaa mpango mpya wa ushirikiano wa kimaendeleo na Tanzania, utakaojielekeza katika kufanikisha agenda mbalimbali za maendeleo ya nchi kupitia programu zake mbalimbali ikiwemo kusaidia mfuko wa maendeleo ya jamii-TASAF, usimamizi wa fedha za umma, biashara na uwekezaji kupitia asasi za kiraina sekta binafsi.
Balozi Didier Chassot, ameitumikia nafasi hiyo ya ubalozi akiwa hapa nchini kwa kipindi cha miaka minne na ameahidi kuendelea kuwa balozi mzuri wa Tanzania atakaporejea nchini kwake kuendelea na majukumu yake mengine.