Mwenendo wa shilingi ni tulivu -Mwigulu

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba amesema mwenendo wa thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya sarafu za nchi washirika wakuu wa kibiashara imeendelea kuwa tulivu, licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali za kiuchumi duniani hususan ongezeko la bei za bidhaa.

Amesema hali hiyo ya utulivu  imetokana na utulivu wa mfumuko wa bei nchini ukilinganishwa na nchi washirika wa kibiashara.

Mwigulu amesema kuwa utekelezaji wa sera thabiti za fedha na bajeti, na uwepo wa chakula cha kutosha nchini.

“Katika mwezi Aprili, 2023 dola moja ya Marekani ilibadilishwa kwa wastani wa shilingi 2,324.07 ikilinganishwa na shilingi 2,322.16 kipindi kama hicho mwaka 2022.”Amesema

Aidha, amesema katika kipindi cha kuanzia Aprili 2022 hadi Aprili 2023 dola moja ya Marekani ilibadilishwa kwa wastani wa shilingi 2,310.14.

Habari Zifananazo

Back to top button