Serikali kubuni vyanzo vipya kusaidia upatikanaji wa Umeme

IRINGA: Serikali imesema itaongeza upatikanaji wa gesi ili kufidia hali ya upungufu wa umeme nchini unaochangiwa na upungufu wa maji kwenye mabwawa yanayozalisha umeme.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk. Doto Biteko wakati alipotembelea mradi wa bwawa la kufua umeme la Mtera ili kujionea hali ya maji kwenye bwawa hilo ambalo limeathiriwa na upungufu wa maji unaosababishwa na ukame kutokana na kuchelewa kwa mvua.
Dk. Biteko amesema Serikali kwa kushirikiana na TANESCO itafanya kila linalowezekana kubuni vyanzo vipya vya upatikanaji umeme ikiwa ni pamoja na gesi ya kutosha ili shughuli za kiuchumi zisiathirike.
Amesisitiza kuwa uchumi wa Wananchi wa Tanzania unategemea sana upatikanaji wa umeme ,hivyo shughuli zozote za kimazingira zikiathiriwa zinaathiri pia hali ya upatikanaji umeme na amewataka Wananchi kutunza vyanzo vya maji na mazingira.

Habari Zifananazo

6 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button