Serikali kuendelea kuimarisha mazingira ya biashara

SERIKALI inaendelea kuweka mazingira rafiki ya biashara ili kuwezesha upatikanaji wa ajira kwa watanzania sanjari na ukuaji wa uchumi ikiwemo uzalishaji wa bidhaa bora zinazouzwa ndani na nje ya nchi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk, Selemani Jafo wakati ziara aliyoifanya katika kiwanda cha magodoro cha Tanfoam kwaaajili ya kutembelea wawekezaji na kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji zinazofanyika.

Advertisement

Dk Jafo amesema serikali inaendelea kuweka mazingira rafiki ya biashara yenye lengo la ukuzaji uchumi na wananchi kupata ajira hususan vijana na wanawake sanjari na kuhakikisha wafanyakazi wanapata stahiki zao

“Serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki ya biashara sanjari na ukuzaji wa uchumi ikiwemo utatuzi wa changamoto mbalimbali kwa wawekezaji lengo kukuza ajira kwa watanzania”.

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Kiwanda cha TANFOAM, Meshack Jimy amesema upanuzi wa kiwanda hicho eneo la Moshono utaongeza ajira kwa watanzania sanjari na ongezeko la mitambo kwani kampuni hiyo kwa hivi sasa inaendesha kiwanda katika hali ya ufinyu wa eneo lakini ujenzi wa kiwanda kipya hadi kukamilika kwake kutawezesha mitambo mipya na mingineyo kusimikwa ili kuongeza uzalishaji zaidi