Serikali kugawa vyandarau bila malipo Shinyanga

SERIKALI inatarajia kugawa vyandarua zaidi ya milioni 1.5 bila malipo kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga lengo kutokomeza maambukizi ya malaria ambayo yamezidi kuenea kwa kasi.

Ofisa kutoka Mpango wa Taifa wa Kuthibiti Malaria (NMCP) Peter Gitanya amesema hayo Januari 6, 2025 katika mafunzo na waandishi wa habari juu ya kampeni ya uhamasishaji wa kugawa vyandarua bila malipo kwenye kaya mkoani Shinyanga.

Advertisement

Gitanya amesema vyandarua hivyo vitaanza kugawiwa Januari 16, 2025 na katika kaya chandarua kimoja watapatiwa watu wawili na vitumike katika malengo yaliyokusudiwa kwa usahihi kwani hapa Tanzania asilimia 93 wananchi wanaishi katika hatari ya kuambukizwa Malaria.

Gitanya amesema uhamasishaji ulianza tarehe 12 na vyandarua hivyo vinadawa kwa mujibu wa wataalamu wa Afya wanadai utumikaji wa vyandarua unapunguza maambukizi ya malaria kwa asilimia 68.

“Mkoa wa Shinyanga una asilimia 16 ya maambukizi ya mnalaria hivyo waandishi watoe elimu iliyo sahihi vyandarua havina madhara kama inavyodaiwa kuwa vinapunguza nguvu za kiume au vinaongeza kuwepo kwa mbu wengi.,”amesema Gitanya.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Faustine Mulyutu amesema waandishi wa habari wanatakiwa kufahamu kwa undani maambukizi ya malaria na dalili zake , kutunza mazingira na kazi ya daktari ni kutibu ni vyema waandishi wakipata uelewa watasaidia kuelimisha jamii namna ya kujikinga.

“lengo letu tujenge shinyanga yetu isiyo na Malaria tuifikie jamii kuipa elimu wanapohisi dalili za Malaria waende kwenye vituo vya kutolea huduma za afya haraka”amesema Mulyutu.

Mratibu wa Malaria Mkoa wa Shinyanga Betty Shayo amesema kweli maambukizi ya malaria yamepungua kwa mkoa wa Shinyanga na itambue mtu mmoja akifariki kwa malaria katika familia anakuwa ameacha pengo kubwa hivyo waandishi wa habari wanayo nguvu zaidi ya kuelimisha jamii juu ya kujikinga ikiwemo kutumia chandarua.