Serikali kuimarisha tiba bobezi – Mhagama

DAR-ES-SALAAM : WAZIRI wa Afya,Jenista Mhagama amesema serikali itaendelea kuimarisha tiba bobezi ili kuokoa maisha ya wananchi na kupunguza rufaa za kwenda nje ya nchi.

Waziri Mhagama aliyasema hayo wakati alipotembelea  Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo muhimbili (MOI)  na kuipongeza taasisi hiyo kwa kupunguza idadi ya wagonjwa wa mifupa, ubongo na mishipa kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Aidha amesema utaratibu ulioko MOI wa  kutenga siku za Jumatano na Ijumaa kwa ajili ya kusikiliza kero, maoni, mapendekezo na changamoto kutoka kwa wagonjwa na ndugu wa wagonjwa  ni njia bora ya kupata mrejesho kutoka kwa wagonjwa wanaopatiwa huduma za kimatibabu na kuboresha huduma kwa wateja.

“Nimekutana na mgonjwa kashafanyiwa oparesheni ya ubongo mara mbili na yupo vizuri, tumeokoa fedha nyingi ambazo serikali ingezitumia kwa ajili ya matibabu, pia tunapunguza mzigo mkubwa kwa wananchi katika kujisimamia kuhangaika kutafuta tiba hizi ambazo ni za kibobezi nje lakini zinakafanyika hapo.

Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI,Dk Lemeri Mchome  amesema kuwa Taasisi ya MOI imeshaanzisha matibabu ya wagonjwa wa kiharusi na tayari imewezesha baadhi ya wataalam kuhudhuria mafunzo nje ya nchi na kuendesha mafunzo ndani ya nchi kwa kuleta wataalam kutoka mataifa ya nje ili kuwajengea uwezo madaktari bingwa wa taasisi hiyo.

“Tunamshukuru Rais wetu Dk Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa wa vifaa tiba ukiachilia mbali rasilimali watu ametoa zaidi ya bilioni 26 ambazo zinatuwezesha sisi kutoa matibabu ya kibingwa na kibobezi ambayo yanatolewa sehemu mbalimbali duniani,” amesema Dk Mchome

Amesema kwa upande wa mifupa zaidi ya asilimia 99 ya magonjwa yote ya mifupa yanatibiwa hapa ndani ya nchi na kwa upande wa ubongo na mishipa ya fahamu zaidi ya asilimia 96 yote yanatibowa ndani ya nchi.

Naye mmoja wa wananchi waliokwenda kutibiwa MOI amesema alikuja   hapo alikuwa haoni lakini sasa anaona na kuwashukuru madaktari wa hapo na serikali kwani amepata matibabu makubwa na ya hali ya juu.

“Tunapa huduma nzuri tunamshukuru Rais wetu, huduma ni nzuri na wagonjwa ni wengi tunawashukuru wahudumu ukifika kama unaumwa nesi akaja kuongea na wewe unafarijika,”amesisitiza.

SOMA : Idara ya kinga mjipange usafi wa majiji

 

Habari Zifananazo

Back to top button