Utunzaji salama vimelea wasisitizwa

WATAALAMU wa maabara nchini wametakiwa kuzingatia kwa umakini mkubwa maadili na viapo vya taaluma yao ili kulinda jamii dhidi ya madhara yanayoweza kusababishwa na utunzaji usio salama wa vimelea hatarishi na smpuli zinazohifadhiwa kwa muda mrefu.

Wito huo umetolewa na Mratibu wa Afya Moja kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Valentino Sanga, wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha siku tano kinachofanyika jijini Arusha kwa lengo la kuimarisha usalama wa maabara na ulinzi wa afya ya jamii.

Sanga amesema mafunzo hayo yanatoa fursa kwa washiriki kubadilishana uzoefu, kujifunza miongozo ya kisasa na kukumbushana wajibu wao wa kitaaluma katika kuzuia na kubaini mapema vihatarishi vya kiafya. SOMA: Tanzania juu Afrika, huduma bora za maabara

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuhifadhi kwa usalama vimelea hatarishi na sampuli za maabara, akionya kuwa uzembe katika utunzaji wake unaweza kusababisha madhara makubwa kwa wataalamu na jamii kwa ujumla.

Jumla ya wataalamu 26 kutoka taasisi mbalimbali za Serikali na sekta ya afya wanashiriki katika mafunzo hayo yanayoungwa mkono na CIHEB-Tanzania kupitia Mradi wa Usalama wa Afya Duniani (GHS), kwa lengo la kuimarisha viwango vya usalama wa maabara nchini.

 

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. 78WIN ngày càng được nhiều anh em quan tâm nhờ kho game đa dạng trải nghiệm mượt mà và nhiều sự kiện ưu đãi diễn ra thường xuyên. Một sân chơi trực tuyến đáng để khám phá 🎯

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily…………
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button