Serikali kuimarisha usalama barabarani

DODOMA: Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Dk Charles Msonde, amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua za haraka kuimarisha usalama barabarani kwa kuboresha usanifu wa miundombinu, kuimarisha utekelezaji wa sheria, pamoja na kuwajengea uwezo wataalamu ili juhudi hizo ziweze kuleta matokeo chanya kwa watumiaji wote wa barabara.

Dk Msonde ametoa kauli hiyo mkoani Dodoma Februari 25, 2026, wakati akifungua mafunzo ya ukaguzi wa usalama barabarani yaliyoandaliwa na Wizara ya Ujenzi kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Lund kutoka Sweden na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia mradi wa AfroSAFE.

Amesema ajali za barabarani bado ni changamoto kubwa ya usalama wa jamii na zinasababisha vifo, majeraha, ulemavu wa kudumu pamoja na uharibifu wa miundombinu na vyombo vya usafiri, hali inayoongeza gharama za matengenezo kwa Serikali na wananchi.

Dk Msonde ametoa rai kwa wataalamu wa mafunzo hayo kushiriki kikamilifu ili mafunzo yawasaidie kuongeza ujuzi na utaalamu wa kihandisi katika masuala ya usalama barabarani pamoja na kubaini mapungufu yaliyopo katika miundombinu ya barabara.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Ujenzi, Eng. Kashinde Mussa, amesema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha Serikali inapunguza ajali za barabarani kwa angalau asilimia 50 ifikapo mwaka 2030.

Ameeleza kuwa takwimu za dunia zinaonesha ajali za barabarani zinaongezeka, ambapo takribani watu milioni 1.19 hupoteza maisha kila mwaka, huku kati ya milioni 20 hadi 50 wakipata ulemavu wa kudumu kutokana na ajali hizo.

Amebainisha kuwa mafunzo hayo yatasaidia kupunguza makosa yanayotokana na miundombinu ya barabara, huku yakilenga kuwajengea uwezo wataalamu kutoka TANROADS na TARURA katika kubuni, kusanifu na kujenga barabara salama zaidi.

Naye, Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Jackline Masaki, amesema mafunzo hayo yatawawezesha wahandisi kupata ujuzi wa kina katika ukaguzi na uchunguzi wa usalama barabarani ili kuhakikisha barabara zinakuwa salama kwa watumiaji wote.

Zaidi ya wahandisi 50 wanashiriki katika mafunzo hayo ya siku tatu mkoani Dodoma

Habari Zifananazo

8 Comments

  1. 👀👀👂👂【Boost your Luck in Betting】Recent data from late 2025 indicates that the betting industry in Tanzania is experiencing a significant boom, with approximately 39.5 million people (roughly 56% of the population) says:

    .

    1. I get paid over (90$ to 200$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $18000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
      .
      HERE——————————————⊃⫸ https://Www.Cash54.Com

    2. I get paid over 220 Dollars per hour working from home with 2 kids at home. i never thought i’d be able to do it but my best friend earns over 15k a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life. This is what I do, check it out by Visiting Following Website…

      .
      M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

  2. Rais amefichua kuwa vurugu za uchaguzi zimeleta Neema ya Mvua na Mazao mengi kunufaisha Taifa

  3. Rais amefichua kuwa vurugu za uchaguzi zimeleta Neema ya Mvua na Mazao mengi kunufaisha Taifa.

  4. Rais amefichua kuwa vurugu za uchaguzi zimeleta Neema ya Mvua na Mazao mengi kunufaisha Taifa

  5. Rais amefichua kuwa vurugu za uchaguzi zimeleta Neema ya Mvua na Mazao mengi kunufaisha Taifa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button