Serikali kukabiliana na kupanda kwa bei za vyakula

ZANZIBAR: RAIS wa Zanzibar, Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali imeanza kuchukua hatua kukabiliana na upandaji wa bei za vyakula hasa mchele na sukari nchini.
Dk.Mwinyi ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wafanyabiashara wanaoagiza vyakula nje ya nchi na watendaji wa Serikalini.
Aidha amesema matarajio ya Serikali ni kurudisha bei za awali kwa bidhaa zilizopo madukani, pia ameagiza Serikali kutoa fedha zake za kigeni na kuwapa kipaumbele wafanyabiashara hususani waagizaji vyakula nje ya nchi, hivyo amewataka wafanyabiashara hao kushirikiana kuagiza bidhaa hizo kwa pamoja.
Vilevile, Rais Dk.Mwinyi amegusia suala la mizigo kushukia bandari ya mkoani ili kupunguza gharama za bidhaa Pemba.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
2
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x