Serikali kutatua changamoto za vijana

DODOMA: WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Ridhiwani Kikwete amesema serikali iko tayari kukutana na vijana kuanzia ngazi za chini za maamuzi ili kukabiliana na changamoto zao kupitia programu mbalimbali.

Kikwete ametoa taarifa hiyo Julai 31, 2024 aliposhiriki Kongamano la Vijana lililoandaliwa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya DOYODO ikishirikiana na wadau mbalimbali jijini Dodoma.

Amesema katika kutekeleza hilo, serikali pia itafanya marekebisho ya sera na sheria ili ziendane na mahitaji yao.

Advertisement

Waziri huyo ambaye ni Mbunge wa Chalinze ametumia jukwaa hilo kuwaeleza vijana juu ya nia ya serikali kuendelea kuwahudumia katika maeneo mbalimbali ya maisha yao.

SOMA: Mabadiliko ya mfumo yarahisishwa kwa vijana

“Pamoja na hayo, nawaahidi vijana kuwa serikali yao itawasikiliza na kuyafanyia kazi mahitaji yao ikiwemo la ajira na mitaji kuwawezesha kufanya biashara na shughuli nyingine za kipato,” alisema Kikwete.

 

/* */