Serikali mbioni kusaini mkataba wa LNG

Sh trilioni 70 kuleta mapinduzi ya kiuchumi

SERIKALI ipo hatua za mwisho za maandalizi ya kusaini mkataba wa  mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia (LNG) na wawekezaji Kampuni ya Shell ya Uholanzi na Equinor ya Norway .

Hayo yamesemwa leo Julai 3, 2023 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba katika mdahalo ulioandaliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), kuhusu mafuta na gesi asilia uliofanyika katika Maonyesho ya 47 ya  Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba).

Amesema, uwekezaji wa mradi huo ni  zaidi ya Shilingi Trilioni 70 utaleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi nchini na utaifanya Tanzania kuwa moja ya nchi zinazochangia katika usalama wa nishati dunia.

Mramba amesema, mradi huo wa kuchimba Gesi Asilia katika eneo la Bahari Kuu Kusini mwa Tanzania katika eneo la Likong’o Lindi utakuwa na faida kubwa kwa nchi, ni mradi ambao serikali inatarajia utabadilisha pato la taifa (GDP).

“Uchumi wa nchi yetu na maisha ya watu yatabadilika. Utazalisha ajira, utatoa fursa ya kuweka viwanda vingine, ni mradi ambao utaongeza kiasi cha gesi ambacho kitatumika ndani ya nchi, na kitakachouzwa nje na kuingiza fedha nyingi za kigeni.” Amesema Mramba

Amesema, gesi asilia ambayo Tanzania imegundua kiasi kikubwa kipo baharini, gharama ya kuitoa Baharini ni kubwa umbali wa kutoka nchi  kavu kuingia ndani ya Bahari mpaka kufika maeneo ya vile visima, ni kati ya kilometa 120 mpaka 250  ni ndani sana na unaikuta gesi ikiwa kwenye kina kirefu cha Bahari.

“Gharama za uwekezaji ni kubwa  lakini huu ndio muda muafaka wa kuvuna rasilimali hiyo ambayo Mungu ameibariki nchi yetu.”Amesema na kuongeza

“Msisahau gesi asilia duniani inatajwa kama nishati mbadala, tunapoelekea dunia inaenda kuhama kutoka kwenye gesi ya hewa  ukaa na kutumia nishati ambazo hazizalishi hewa ya ukaa. matumizi ya mafuta na gesi tunapokwenda yataenda kupungua.

Habari Zifananazo

3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button