Serikali, sekta binafsi kuwakwamua wanawake

DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk Dorothy Gwajima amesema serikali itaendelea kuungana na sekta binafsi kumkwamua kumuwezesha mwanamke kiuchumi.

Dk Gwajima amesema hayo leo Mei 12, 2025 jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya kuwashukuru wadhamini na kamati ya kitaifa ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani 2025 iliyofanyika Machi 8 mkoani Arusha iliyoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Aidha, Dk Gwajima amesema ili maendeleo yafike kwa jamii ni lazma kuwe na fikra kwanza ili wanaopelekewa maendeleo hayo wajue nini kina kuja na kina tija gani kwao na kwa jamii husika hivyo sherehe hiyo haikuwa kusherehekea tu bali ilikuwa ni kutathmini mafanikio ya kiuchumi, kisiasa pamoja na kudumisha ushirikiano baina ya serikali na sekta binafsi.

 

Gwajima amesema wanawake wanapaswa wajiunge na majukwaa mbalimbali ya kiuchumi na kuweza kujinasua na wimbi la umaskini kwa jamii.

Awali akizungumza Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake, Sarah Masasi ameshukuru kwa wafadhili hao kufadhili siku hiyo kwani mwanamke ni mtu muhimu kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Naye mwakilishi wa wadhamini kutoka, Equity Benki ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Isabela Maganga amesema wataendelea kujumuika na wizara hiyo pamoja na serikali na wasisite kuwajuza kama kutakuwa na jambo lingine

Maadhimisho hayo yaliyofanyika mkoani Arusha zaidi ya bilioni 1 zilichangwa na wadau mbalimbali pamoja na wadhamini waliojitokeza kudhamini maadhimisho hayo.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button