Serikali kutoa taarifa ya Covid-19

Yataka wananchi kutulia

WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu amesema serikali inafuatilia tetesi za uwepo wa Covid 19 nchini.

Akitoa taarifa kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii amewaondoa hofu  wananchi na kuwaomba  kutulia wakati wanafuatilia suala hilo.
“Wizara ya Afya inachakata taarifa zilizokusanywa kutoka Hospitali/Vituo mbalimbali ndani ya wiki hii tutatoa taarifa kama kuna ongezeko la magonjwa ya mfumo wa hewa au lah!” Amesema Ummy na kuongeza

“Kwa taarifa za wagonjwa waliopimwa virusi vya Covid-19 wiki ya kuanzia May 6 hadi Mei 12, 2023, watu sita kati 6  ya 288 walithibitishwa kuwa na corona ikiwa ni pungufu ikilinganishwa na wiki ya April 29 hadi May 05,2023, hakuna kifo chochote kilichothibitishwa kusababishwa na Covid-19. “AmesemaAmesema, wizara ya afya inaendelea kufuatilia kwa karibu kwenye Hospitali mbalimbali na kwamba watatoa taarifa kamili.

“Nawaomba wananchi muendelee kuzingatia kanuni za afya na usafi.

“Amesema

Habari Zifananazo

Back to top button