Serikali: Wasiokuwa na dharura wakae nyumbani
SERIKALI imeagiza wananchi wasio na dharura kesho Desemba 9, 2025 washerehekee miaka 64 ya Uhuru wa Tanzania Bara wakiwa nyumbani.
Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba akitoa salamu za Uhuru kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan katika taarifa aliyoitoa kwa vyombo vya habari leo Desemba 8, 2025 amesema ni vyema wananchi wasio na dharura wakakaa nyumbani.
“Serikali inawashauri wananchi wote ambao siku hiyo hawatakuwa na dharura, kusherehekea wakiwa nyumbani isipokuwa kwa wale ambao majukumu yao wanawataka kuwepo katika vituo vyao vya kazi kama watakavyoelekezwa na viongozi wao,” amesema Dk Mwigulu.



