RAMAPHOSA : Serikali ya Muungano inayumba

JOHANESBURG : SERIKALI  ya muungano wa kitaifa ya Afrika Kusini inakumbwa na mizozo kutokana na tofauti kati ya vyama tanzu vinavyounda serikali, lakini Rais Cyril Ramaphosa ameahidi kuwa serikali hiyo ni thabiti.

Rais Ramaphosa anatarajiwa kulihutubia taifa leo kuhusu utendaji kazi wa serikali hiyo, kwa mara ya kwanza tangu kuundwa kwake.

Mizozo kadhaa imejitokeza ndani ya serikali, ikiwa ni pamoja na mpango wa kufundisha lugha ngeni shuleni na uhusiano wa karibu kati ya Ramaphosa na utawala wa Russia, ambayo imetishia kuisambaratisha serikali.

Pia, mzozo umeibuka baada ya Rais Ramaphosa kusaini sheria inayoiwezesha serikali kumiliki mashamba kutoka kwa watu binafsi kwa maslahi ya umma, bila kulipa fidia. Hata hivyo, Rais Ramaphosa amepuuza madai ya kuwepo kwa mpasuko katika serikali yake, akisema yanayoelezwa si sahihi na kwamba viongozi wanajadili masuala hayo kwa pamoja.

SOMA: Afrika Kusini yajivunia mchango wa Hayati Nyerere

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button